KAMATI YA BUNGE YAPONGEZA UWEKEZAJI KIWANDA CHA MKULAZI
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii, Mhe. Fatma Toufiq amepongeza uwekezaji uliofanywa katika kiwanda cha sukari cha Mkulazi. Mhe. Fatma ametoa pongezi hizo katika ziara ya kamati hiyo ya kukagua maendeleo ya kiwanda hicho kilichojengwa na Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) kwa ubia na Jeshi la Magereza mwishoni mwa wiki.