
MKULAZI HOLDING COMPANY LIMITED

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa Daniel Chongolo ameridhishwa na hatua iliyofikiwa ya mradi wa ujenzi wa kiwanda cha sukari kilichopo Mbigiri Wilaya ya Kilosa Mkoa wa Morogoro mara baada ya kutembelea ujenzi wa kiwanda hicho akiongozana na Viongozi wengine wa Chama hicho.
Ameyasema hayo Januari 30,2023 wakati akizungumza na Uongozi wa kiwanda hicho kinachomilikiwa na Kampuni Hodhi ya Mkulazi .
Katibu Mkuu Chongolo amesema miradi kama hii ikibuniwa na kutekelezwa ina tija kubwa sana kwani inaweza kutoa ajira kwa vijana wakitanzania.
“Nimefurahishwa sana kuona vijana wote wataalamu ni wa kitanzania” alisema Katibu Mkuu Chongolo.
Pia Katibu Mkuu Chongolo alitoa wito kwamba sukari itakayozalishwa na kiwanda hiki ienda kushusha bei ya sukari kwa walaji.
Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Kampuni Hodhi ya Mkulazi Selestine Some alisema Kiwanda cha Sukari kilichopo Mbigiri kinatarajia kuzalisha sukari Juni mwaka huu.
Ujenzi wa Kiwanda hicho ulianza Julai 2021 ambao unatekelezwa kwa ubia kati ya Shirika la Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kwa kushirikiana na Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Magereza(SHIMA).