Image

MKULAZI HOLDING COMPANY LIMITED

Image
KUKAMILIKA KWA UJENZI WA KIWANDA CHA SUKARI MBIGIRI

KUKAMILIKA KWA UJENZI WA KIWANDA CHA SUKARI MBIGIRI

Ujenzi Kiwanda cha Sukari Mbigiri kilichopo wilaya ya Kilosa Mkaoni Morogoro umefikia asilimia 55 ambapo kinatarajiwa kuanza kuzalisha sukari hivi karibuni. Kiwanda hicho kina ukubwa wa eneo la hekta  4,856, kati ya hizo eneo la hekta 3,600 zitalimwa na kupandwa miwa. Tayari eneo lenye ukubwa wa hekta  2,810 limeshapandwa miwa ambalo ni sawa na asilimia 78% ya lengo la hekta 3,600.

Uwepo wa kiwanda  katika  eneo hilo umetoa fursa hasa kwa wakulima wanaozunguka eneo hilo ambapo wakulima 243 wamesajiliwa  na Bodi ya Sukari nchini kwa kulima miwa kwa ajili ya malighafi  ya kiwanda hicho. Kiwanda  kitakapomalizika kinatarajiwa kuzalisha tani 50,000 kwa mwaka.

Huu ni uwekezaji mkubwa unaofanywa na Serikali kwa lengo la kukabiliana na upungufu wa sukari nchini. Kiwanda cha Sukari Mbigiri  kinamilikiwa na Kampuni Hodhi ya Mkulazi  chini ya ubia wa  Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii(NSSF) na Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Magereza (SHIMA).