
MKULAZI HOLDING COMPANY LIMITED

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako ameipongeza Kampuni Hodhi ya Mkulazi kwa kazi nzuri ya ukulima wa miwa ambayo itatumika kama malighafi ya kuzalisha sukari kwenye kiwanda cha Sukari Mbigiri. Ametoa pongezi hizo tarehe 21 Julai,2022 Wilaya ya Kilosa wakati ...
Serikali imehimiza mkandarasi anayesimamamia kazi ya ujenzi Kiwanda cha Sukari Mkulazi kufanya kazi hiyo ndani ya muda ulioweka kwenye Mkataba.
Amewaagiza Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama, Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Nchemba, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tixon Nzunda wakutane ili wakamilishe taratibu za utoaji wa mitambo ya ujenzi wa kiwanda cha Sukari cha Mbigiri.
Ujenzi Kiwanda cha Sukari Mbigiri kilichopo wilaya ya Kilosa Mkaoni Morogoro umefikia asilimia 55 ambapo kinatarajiwa kuanza kuzalisha sukari hivi karibuni. Kiwanda hicho kina ukubwa wa eneo la hekta 4,856, kati ya hizo eneo la hekta 3,600 zitalimwa na kupandwa miwa. Tayari eneo lenye ukubwa wa hekta 2,810 limeshapandwa miwa ambalo ni sawa na ...